Mark 2:1-6

Isa Amponya Mtu Aliyepooza

(Mathayo 9:1-8; Luka 5:17-26)

1 aBaada ya siku kadhaa Isa alirudi Kapernaumu, watu wakasikia kwamba amerudi nyumbani. 2 bHivyo watu wengi wakakusanyika kiasi kwamba hapakubaki nafasi yoyote hata mlangoni! Naye akawahubiria Neno. 3 cNdipo baadhi ya watu wakaja wakamletea Isa mtu aliyepooza, akiwa amebebwa na watu wanne. 4Kwa kuwa walikuwa hawawezi kumfikisha kwa Isa kwa ajili ya umati wa watu, walitoboa tundu kwenye paa mahali pale alipokuwa Isa, wakamshusha yule aliyepooza kwa kitanda alichokuwa amelalia. 5 dIsa alipoiona imani yao, alimwambia yule mtu aliyepooza, “Mwanangu, dhambi zako zimesamehewa.”

6Basi baadhi ya walimu wa sheria waliokuwa wameketi huko wakawaza mioyoni mwao,
Copyright information for SwhKC